Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere

"Inaunganisha Tanzania na Dunia "
TAA Logo

Malikale

Imewekwa: 12 July, 2024
Malikale

Historia ya uhifadhi wa malikale ilianza mwaka 1937 ilipoanzishwa Sheria ya Uhifadhi wa Majenzi ya Kihistoria (Monument Preservation Ordinance, 1937).Wakati huo uhifadhi wa malikale ulijihusisha zaidi katika kutafuta na kuorodhesha kumbukumbu za kihistoria hasa katika maeneo ya mwambao yaliyohusiana na utawala wa kikoloni, hususan majengo na makaburi.

Mwaka 1964, Sheria ya Mambo ya Kale Na.10 ilitungwa na kuchukua nafasi ya ‘Monument Preservation Ordinance ya mwaka 1937. Aidha, mwaka 1979 Sheria hii ilifanyiwa mapitio ambayo yalipanua wigo wa kuhifadhi na kulinda malikale kwa kujumuisha maeneo na vitu vya kipaleontolojia, akiolojia, historia,vitu vya asili.na kuanzishwa kwa baraza la ushauri wa malikale.