Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA)

TFRA Logo
Wakulima 2500 wa vitunguu wanufaika na ruzuku ya mbolea Karatu, serikali yapongezwa
29 May, 2024
Wakulima 2500 wa vitunguu wanufaika na ruzuku ya mbolea Karatu, serikali yapongezwa

Wakulima 2500 wa vitunguu wilayani Karatu wamenufaika na mpango wa mbolea za ruzuku tangu kuanza kwake mwezi Agosti 2022 mpaka Januari 2023.

Mpango huo umesaidia sana kupunguza gharama za uzalishaji wa zao hilo kufuatia kiasi cha mifuko 12 kutumika kwa heka moja ya vitunguu.


Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, Karia Magaro alipokuwa akizungumza na wanahabari kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) waliofika ofisini kwake kufuatilia manufaa yaliyotokana na mpango wa ruzuku kwa mwaka wa fedha, 2022/2023.


"Suala la ruzuku za mbolea limepokelewa kwa furaha sana na wakulima na limekuja kwa wakati.

Nimpongeze sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali sana wakulima na waziri wa kilimo, Hussein Bashe kwa kuratibu Mfumo wa mbolea za ruzuku" Magaro alisema .

Mbolea Day