Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Nishati

Gas Company (Tanzania) Limited

Kituo cha Makutano cha Somanga

Imewekwa: 03 January, 2024
Kituo cha Makutano cha Somanga
Kituo cha makutano cha Somanga kinapatikana katika kijiji cha Somanga ndani ya Mkoa wa Lindi. Kituo hicho kinatumika kama sehemu muhimu ambapo mabomba ya gesi yanayotoka viwanda vya kuchakata gesi vya Madimba na SongoSongo yanakutana na kuungana na bomba moja kuendelea na safari yake kwenda katika kituo cha kupokelea gesi cha Dar es Salaam. Inafanya kazi kama karakana kuu ya matengenezo ya miundombinu ya bomba zima la gesi, kituo hiki kina umuhimu wa kimkakati.
Kando na jukumu lake la urekebishaji, Kituo cha Makutano cha Somanga kimetengwa kama sehemu ambayo hapo mbeleni zitasimikwa kopresa ili kuongeza shinikizo la bomba itakayowezesha kukidhi ongezeko la mahitaji ya siku zijazo.