JIJI LA ARUSHA LAZINDUA MITAMBO MIPYA
JIJI LA ARUSHA LAZINDUA MITAMBO MIPYA
Imewekwa: 20 November, 2025
Jiji la Arusha limezindua mitambo mipya ikiwa ni Malori mapya mawili na Mtambo mmoja kwa ajili ya ukarabati na kutengeneza barabara za ndani ya Jiji la Arusha na kulifanya Jiji liwe na miundombinu bora inayopitika majira yote. Akizindua mitambo hiyo,Mstahiki Meya,Mhe. Maxmillian Iraqnhe amesema mitambo hioyo itakarabati barabara zote za Arusha ambazo ni za ndani ili kuboresha miundo mbinu ambayo hivi karibuni ilikuwa ina changamoto.Naye Mkurugenzi wa Jiji Ndg. John L. Kayombo amewahakikishia wananchi wa Arusha kuwa sasa changamoto ya Miundombinu imepata muarobani.Mitambo yote hiyo mitatu imegharimu pesa za kitanzania Tshs. 1.7 Bilioni