Eneo la waliponyongwa Mashujaa wa Vita ya Majimaji
Eneo hili linafahamika zaidi kama manyongeo ni eneo maarufu na la kihistoria unapofika ndani ya mji wa Songea katika eneo hili ndio mahali palipotumika tangu enzi za ukoloni na ndio eneo ambalo lililotumika kunyongea mashujaa 66 waliopigana kipindi cha vita vya Majimaji, eneo hili la manyongeo limekuwa eneo la kumbukumbu zaidi kwa jamii ya watu wa Songea na mkoa wa Ruvuma kwa ujumla hasa kwa wahanga wa vita vya Majimaji ndio sehemu ambayo wananchi walikusanyika na kushuhudia mababu, baba, wajomba na ndugu zao wengine wakinyongwa na Mjerumani mpaka kifo.
Majina ya mashujaa wa vita vya Majimaji kwa upande wa Tanganyika waliozikwa kwenye kaburi moja (kaburi la halaiki)
Moja kwati ya Kamba/Kitanzi kilichotumika kunyongea Mashujaa wa Vita ya Majimaji
Karibu Kituo cha Makumbusho ya Vita ya Majimaji - Songea kupata kujua idadi ya majina yote 66 ya Mashujaa walionyongwa, Kuona kaburi la Halaiki pamoja na kupata historia ya vita ya majimaji kwa ukubwa wake.
Mawasiliano:
Majimaji Memorial Museum
P.O BOX 1249 Songea,
Tanzania
Mobile: +255 786 472700
Email: majimaji@nmt.go.tz