MAKUMBUSHO YA TAIFA YAKABIDHI NGAO YA SHUKRANI KWA TPDC KWA UFADHILI WA MWL. NYERERE MARATHON 2023
Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa la Tanzania, Dkt.Noel Lwoga amekabidhi ngao ya shukrani kwa uongozi wa Shirika la Maendeleo ya Mafuta Tanzania (TPDC) kwa kutambua mchango wa Taasisi hiyo katika Mbio za hiari zijulikanazo kama Mwl. Nyerere Marathon zilizofanyika Septemba mwaka jana huko Butiama, Mkoani Mara.
Ngao hiyo imekabidhiwa Machi 15 2024 jijini Dar es Salaam kwa Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa TPDC Bi.Maria Mselemu kwa niaba ya Mkurugenzi wa Shirika hilo.
Akizungumza wakati wa kukabidhi ngao hiyo, Dkt. Lwoga ameishukuru TPDC kwa mchango wao katika kuendeleza, kutangaza na kusherehekea urithi wa Mwl. Nyerere kupitia mbio za hizo za hiari.
Naye Mkuu wa Kitengo Uhusiano na Mawasiliano wa TPDC, Bi Maria Mselemo alishukuru kwa jinsi taasisi yake ilivyoshirikishwa katika mbio hizo na kwamba wako tayari kuendelea kushirikia na Makumbusho ya Taifa kwa lengo la kuendeleza na kutangaza urirhi wa Mwl. Nyerere.