MAAFISA WANAMICHEZO ZAIDI YA MIA TATU KUTEMBELEA MAKUMBUSHO
MAAFISA WANAMICHEZO ZAIDI YA MIA TATU KUTEMBELEA MAKUMBUSHO
Imewekwa: 31 Jan, 2024
Siku ya tarehe 30/1/2024 baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Itifaki ya Baraza la michezo la Majeshi Duniani (CISM) wakiwa wameambatana na Maafisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) wametembelea kituo Cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni jijini Dar es salaam kwaajili ya maandalizi ya ugeni wa Wanajeshi Wanamichezo zaidi ya mia tatu kutoka maeneo mbalimbali duniani wanaotarajiwa kutembelea kwenye vituo vya Makumbusho na maeneo mengine ya Utalii baadae mwezi Mei mwaka huu 2024