Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA MWANDISHI MKUU WA SHERIA

Majukumu ya OCPD

.

Majukumu ya Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria ni:

  1. Kushauri Wizara, Idara huru, Wakala za Serikali , taasisi nyingine za Serikali pamoja na mashirika ya umma juu ya mchakato wa utungaji sheria.
  2. Kumshauri Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusiana na fasiri sahihi ya Sheria Kuu, sheria ndogo na hati nyingine za kisheria.
  3. Kupokea maelekezo ya uandishi wa sheria kutoka katika wizara na kuyafanyia kazi ipasavyo.
  4. Uandishi wa mapendekezo ya kisheria katika Miswada kwa ajili ya utungaji wa sheria.
  5. Uandishi wa hati zote za kisheria na maazimio ya Bunge kwa ajili ya uridhiwaji wa Mikataba ya Kimataifa.
  6. Kushauri wizara ipasavyo kuhusu mpango wao wa mwaka wa fedha wa utungaji wa sheria.
  7. Kuwezesha uwasilishaji wa sheria zilizopitishwa na Bunge katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar, kupitia Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
  8.  
  9. Kutoa ushauri kuhusiana na mchakato wa utungaji wa sheria kwa Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala za Serikali pamoja na Taasisi nyingine za Serikali na Mashirika.
  10. Kutoa ushauri kwa Mwanshaeria Mkuu wa Serikali kuhusiana na maana iliyokusudiwa katika sheria kuu ya Bunge, sheria ndogo na hati nyingine za kihseria.
  11. Kupokea na kutekeleza ipasavyo maelekezo ya uandishi wa Sheria yanayotokana na maamuzi ya Baraza la Mawaziri kutoka Wizarani.
  12. Kuandaa mapendekezo ya sheria kuwa miswada kwa ajili ya kutungwa kuwa sheria.
  13. Kuandaa hati za kisheria na maazimio kwa ajili ya kuridhiwa na Bunge.
  14. Kupokea na kushauri Wizara ipasavyo kuhusiana na kalenda ya utungaji wa sheria kwa kila mwaka wa fedha.
  15. Kuwezesha uwasilishaji wa Sheria zilizopitishwa na Bunge ambazo zinatumika katika pande zote za Muungano kwa Baraza la wawakilishi kupitia Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
  16. Kuandaa au kuhakiki sheria ndogo zinazopendekezwa.
  17. Kutafsiri sheria kuu na sheria ndogo.
  18. Kurekebu sheria kuu na sheria ndogo.
  19. Kuandaa na kuwasilisha kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali taarifa ya kila mwezi katika masuala na majukumu yaliyotekelezwa na Mwandishi Mkuu wa Sheria kwa ajili ya mwongozo na maelekezo.
  20. Kutekeleza jukumu lingine lolote ambalo ni la lazima katika utekelezaji wa majukumu ya ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria kwa kuzingatia Sheria ya utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Sura ya 268.