Another Article
Hifadhi za Bahari hujumuisha maeneo tofauti ndani ya bahari, mito, mabwawa ya asili,na maziwa ambayo ya meteuliwa kisheria
kuweka hatua thabiti za usimamizi zinazolenga kuhifadhi, kuhifadhi, na kurejesha bioanuwai na mifumo ya ikolojia. Hatua hizi
zinahakikisha matumizi endelevu ya rasilimali za baharini, ikiwa ni pamoja na samaki, miamba ya matumbawe, mikoko na nyasi baharini.
Uhifadhi wa maeneo ya bahari ulianza tangu miaka ya 1970 kupitia Sheria ya Uvuvi Na. 6 ya mwaka 1970 na usimamizi wake ulikuwa chini ya Idara ya Uvuvi.
Mnamo mwaka 1994 Serikali kupitia Bunge ilitunga Sheria ya Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Na. 29 ya mwaka 1994 (marejeo 2009 sura 146) ambayo
ilianzisha Kitengo cha Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu kwa ajili ya kuanzisha, kusimamia, kufuatilia na kuendeleza hifadhi za bahari.