- Kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya mawasiliano katika maeneo ya vijijini na maeneo ya mijini yenye mawasiliano hafifu;
- Kuhamasisha ushiriki wa sekta binafsi na serikali katika utoaji wa huduma za mawasiliano kwa wote katika maeneo ya vijijini na maeneo ya mijini yenye mawasiliano hafifu;
- Kuhamasisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika maeneo ya vijijini na maeneo ya mijini yenye mawasiliano hafifu;
- Kutengeneza mfumo kwa ajili ya upatikanaji wa mitandao ya mawasiliano na huduma rahisi na zenye ufanisi katika uzalishaji na upatikanaji katika soko la kiushindani;
- Kuhamasisha utoaji wa huduma bora katika viwango nafuu na kuhakikisha kuwa teknolojia ya habari na mawasilianpo inapatikana vijijini na sehemu za mijini zenye mawasiliano hafifu kwa bei nafuu; na
- Kuhakikisha upatikanaji wa huduma za wote kwa kuboresha upatikanaji wa huduma za mawasiliano kupitia ushiriki wa sekta binafsi.