Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Bodi ya Pamba Tanzania

MAONESHO YA NANENANE YAFANYIKA KANDA YA ZIWA

Imewekwa: 25 August, 2025
MAONESHO YA NANENANE YAFANYIKA KANDA YA ZIWA

PICHANI : Wakulima wa kijiji cha Rungwe Mpya wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, wakifuatilia sherehe za uzinduzi wa msimu wa ununuzi wa pamba 2023/24

Akihutubia katika halfa hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Isaac Mwakisu aliyemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kigoma ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi aliipongeza Bodi ya Pamba Tanzania kwa kutambulisha teknolojia mpya ya upuliziaji viuadudu kwa kutumia ndege zisizo na rubani.

Kanali Mwakisu alisema kuwa “wakulima wa pamba hasa wenye mashamba makubwa wamekuwa na changamoto ya kudhibiti wadudu waharibifu kwa ufanisi kutokana na matumizi ya mabomba ya mgongoni kutokuendana na maeneo wanayo yahudumia hivyo ujio wa teknolojia hii utatatua tatizo hilo na kuwavutia wakulima wengi zaidi kuongeza maeneo ya uzalishaji”