Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Bodi ya Pamba Tanzania

Dira na Dhima

DIRA

Taasisi inayoongoza, kuhamasisha na kukuza ushindani ndani ya tasnia ya pamba kwa kuzingatia ubora, tija na uzalishaji.

DHAMIRA

Kuboresha uzalishaji, tija na faida kwa kuongeza ufanisi katika kusimamia sheria, kanuni na taratibu zinazolinda ubora wa pamba inayozalishwa na kuuzwa ndani na nje ya nchi; kutoa huduma kwa wadau kwa ufanisi zaidi; kukuza ushirikiano na uhusiano miongoni mwa wadau kwa lengo la kujisimamia wenyewe katika kuhamasisha uzalishaji, usindikaji na matumizi ya pamba ndani ya nchi.

MISINGI YA UTENDAJI

  1. Kukuza Kipato
  2. Kukuza Ushirikiano wa Kisekta Maendeleo endelevu
  3. Weledi  
  4. Ubunifu