Mabasi Ya Express
Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), unatoa huduma ya mabasi ya haraka (express) katika Njia Kuu ya Mabasi Yaendayo Haraka ambayo kwa kawaida husimama baadhi ya vituo kutokea katikati ya mji kuelekea Kituo Kikuu cha Kimara na vivyo hivyo kutokea Kimara kuelekea katikati ya mji.
Vilevile Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka unatoa huduma ya Mabasi ya haraka kutokea Njia Mlishi katika Kituo cha Mbezi Luis na Kibaha hadi katikati ya Mji kupitia Njia Kuu.
Huduma hii ya mabasi ya haraka hutambulika kirahisi na abiria aliyeko nje ya basi kwa maandishi ya herufi kubwa yanayoonekana pande zote za basi juu ya vioo vya madirisha. Aidha maandishi hayo pia yanaonekana kirahisi ndani ya basi kupitia vibao maalum vunavyoonyesha uelekeo wa basi husika.
Vituo vya mabasi ya haraka ni kama inavyoonekana katika jedwali lifuatalo;
KIMARA - KIVUKONI |
KIMARA - GEREZANI |
KIVUKONI - KIMARA |
GEREZANI - KIMARA |
|
|
|
|
MBEZI LUIS – KIVUKONI |
MBEZI LUIS - GEREZANI |
KIVUKONI – MBEZI LUIS |
GEREZANI – MBEZI LUIS |
|
|
|
|
MBEZI LUIS – HOSPITALI YA MUHIMBILI |
HOSPITALI YA MUHIMBILI – MBEZI LUIS |
|
|
KIBAHA – GEREZANI (SAA 12:00 ASUBUHI) |
KIBAHA – GEREZANI (SAA 12:30 ASUBUHI) |
|
|