Utekelezaji wa Awamu ya Tatu ya Mradi wa DART unapita katika maeneo ya Bararaba ya Nyerere kutoka Gongolamboto kwenda City Centre na baadhi ya eneo la Barabara ya Uhuru kutoka Tazara kwenda Kariakoo mpaka Gerezani ambao una jumla ya Kilomita 23.6.e Three of DART corridor covers Nyerere Road from Gongo la Mboto to City Centre and Part of Uhuru road from TAZARA to Kariakoo - Gerezani with a total of 23.6 km
Serikali ya Tanzania imepata fedha kutoka International Development Association (IDA) chini ya Benki ya Dunia (WB) kwaajili ya utekelezaji Mradi wa Uboreshaji wa Usafiri jijini Dar es Salaam (DUTP) na inakusudia kutumia sehemu ya fedha hizo za mkopo kulipia gharama stahili chini ya mkataba wa ujenzi wa mfumo wa Mabasi Yaendayo Haraka, ambao ni Awamu ya Tatu ya Mradi wa DART. Hivi sasa washauri wa usimamizi, M/s DOHWA Engineering Co. Ltd na UNITEC Civil Consultants Ltd wanaakiki usanifu na kutayarisha zabuni kwa wakandarasi.