Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji

"Udhibiti wa Haki kwa Matokeo CHANYA"
Utoaji wa leseni na vibali vya ujenzi

Utoaji wa leseni na vibali vya ujenzi

Vibali vya ujenzi

EWURA ina jukumu la kutoa idhini kwa ajili ya ujenzi  wa miundombinu yoyote inayohusika na mkondo wa kati na wa chini wa sekta ndogo ya mafuta. Mtu yeyote anayekusudia kuwekeza katika miundombinu ya sekta ndogo ya mafuta anapaswa kutuma maombi EWURA ili kupata kibali cha ujenzi. Wakati wa kutoa kibali cha ujenzi, EWURA huzingatia masuala ya kiufundi, mazingira, afya na usalama.

Maombi ya kibali cha ujenzi hufanyika kupitia mfumo wa kieletroniki ujulikanao kama License and Order Information System (LOIS). Mwombaji anatakiwa kutuma kwenye mfumo nyaraka muhimu kama ilivyoelezwa katika mwongozo kwa waombaji wa leseni za petroli na idhini ya ujenzi.

Ikumbukwe kwamba, kibali cha ujenzi si leseni. Baada ya kukamilika ujenzi wa miundombinu ya mafuta, mwombaji anapaswa kuomba leseni ya uendeshaji wa miundombinu husika kupitia LOIS. Mchakato wa kutoa leseni ya bidhaa za petroli huanza pale mwombaji anapotuma maombi kamili kwenye mfumo.

Aina za leseni

Zifuatazo ni aina za leseni za mafuta (mkondo wa kati na wa chini) zinazotolewa na EWURA:-

Mwongozo wa maombi ya leseni na vibali vya ujenzi

Baada ya kuwasilisha maombi yaliyokamilika, Mamlaka hufanya yafuatayo: –

  • Kutangaza maombi ya leseni kwenye gazeti ili kupata maoni ya umma endapo wanaridhia maombi hayo ama la;
  • Ukaguzi wa awali wa miundombinu ili kujiridhisha endapo vigezo na masharti vimezingatiwa;
  • Kuandaa ripoti ya tathmini ya maombi na kuiwasilisha katika vikao vya Bodi kwa ajili ya kutoa uamuzi wa kupewa leseni ama la; na,
  • Mwombaji atajulishwa kuhusu uamuzi wa Bodi.

EWURA itatoa leseni ndani ya siku 60 tangu tarehe ya kupokea maombi yaliyokamilika iwapo, itaridhika kwamba, masharti yote ya leseni yamezingatiwa kwa mujibu wa Kifungu cha 133 (1) cha Sheria ya Petroli, Sura ya 392.

Orodha ya leseni ni kama inavyoonyeshwa: –