- Kuwapatia Watanzania fursa za kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi;
- Kuandaa Mpango Mkakati wa sekta na kisekta na kuhamasisha matumizi ya rasilimali kwa shughuli za Uwezeshaji wa Wananchi;
- Kuhamasisha na kuhimiza uwekaji wa akiba, uwekezaji, na ushirikishwaji makini wa Wananchi kwenye shughuli za Kiuchumi;
- Kuandaa Mkakati wa kitaifa Uraghibishi wa sekta mbalimbali wa shughuli za uwezeshaji wananchi kiuchumi;
- Kuendeleza na kuwezesha shughuli za kibiashara zilizoanzishwa na kuendeshwa na watanzania;
- Kuainisha fursa za mafunzo ya kiuchumi na uwekezaji na kuratbu programu za mafunzo hayo;
- Kusimamia, kuongoza na kutafuta vyanzo vya fedha kwa ajili ya Mfuko wa Uwezeshaji;
- Kuhamasisha utafiti wa shughuli za kiuchumi na kuhimiza ushirikiano na Taasisi za utafiti;
- Kufanya mapitio ya sheria mbalimbali kwa lengo la kutoa mapendekezo ambayo yatalenga kuboresha mazingira ya uwezeshaji wananchi kiuchumi;
- Kuandaa mfumo wa kufuatilia maendeleo ya shughuli za kiuchumi na kutathimini matokeo; na mfumo wa menejimenti ya habari za uwezeshaji;
- Kushauri kwenye shughuli zote za uanzishaji wa vikundi, ushirika, ushirikiano na ushirikiano wa biashara wa muda mfupi;
- Kuanzisha mfumo wa utoaji taarifa za uwezeshaji wa wananchi kiuchumi kutoka sekta zote.