Programu ya Imarisha Uchumi na mama Samia (IMASA)
Maana na lengo la Programu
Programu ya Imarisha Uchumi na mama Samia (IMASA) imeanzishwa kwa lengo la kuwawezesha Wanawake, Vijana, Wazee na Makundi Mengine Maalum, IMASA ina tekelezwa katika mikoa 26 ya Tanzania Bara na mikoa 5 ya Zanzibar.
Programu ya IMASA pia ina lengo la kuwawezesha wananchi kwa kuzingatia rasilimali na malighafi zinazopatikana katika mkoa au eneo husika, mathalani wafugaji watawezeshwa kwenye ufugaji, halikadhalika wakulima na wachmbaji madini.
Kazi ya Baraza
Kazi kuu ya Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) ni kuratibu shughuli za uwezeshaji wananchi kiuchumi nchini, ikiwa ni pamoja na kupitia mifuko na program mbalimbali ya uwezeshaji, ushiriki wa watanzania katika uwekezaji, uendelezaji wa wajasiriamali, na uratibu wa shughuli za uwezeshaji katik mikoa na halmashauri mbalimbali hapa nchini. Vile vile Baraza linaratibu na kusimamia kuanzishwaji na uendelezwaji wa vituo vya uwezeshaji nchini. Hadi sasa kuna vituo 25 vya Uwezeshaji nchi nzima ambavyo kazi ya vituo hivyo ni kusimamia, kuratibu na kutoa elimu kwa wananchi juu ya fursa mbalimbali za uwezeshaji nchini.
Baraza lina Waratibu katika maeneo ya miradi yote mikubwa nchini ikiwa na lengo la kusimamia ushirikishwaji na ushiriki wa wananchi katika shughuli za kimaendeleo. Moja ya wajibu wa Baraza ni kuandaa mikakati na miongozo mbalimbali ya uwezeshaji nchini kwa lengo la kuondoa urasimu na kurahisisha shughuli za kiuchumi nchini. Baraza linasimamia vikundi mbalimbali vya wajasiriamali nchini pamoja na kuwaunganisha na fursa mbalimbali za kibiashara zinzopatikana ndani na nje ya nchi.
Nishati safi ya Kupikia
Mheshimiwa Rais Samia ni Champion wa nishati safi ya kupikia, katika azimio la kizimkazi, Mhe. Rais ameonesha kwa vitendo namna anavyowajali wanawake kwa kuhakikisha wanapata nishati safi ya kupikia inayotunza mazingira.
Programu ya IMASA itaweza pia kuibua vipaji katika makundi yote kulingana na mazingara husika, makundi ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu wachangamkie fursa ya IMASA. Lengo la Mhe. Rais Samia na Serikali yake kuanzisha Majukwaa haya ya Uwezeshaji ni kuweza kuwainua wananchi kutoka katika uchumi wa chini kwenda kwenye uchumi wa kati katika kuhakikisha Taifa linakuwa na nguvu kazi imara kwa maendleo ya nchi yao.
Lishe Bora
Vilevile Serikali inayoongozwa na Rais Samia, katika harakati za kuondoa udumavu wa afya na kuboresha lishe katika nchi, inatekeleza Programu ya lishe bora kwa watoto katika ngazi ya vijiji hadi Taifa.
M-MAMA
Mheshimiwa Rais ameanzisha program ya Afya kwa akina Mama inayoitwa M-MAMA ambayo sasa mama Mjazito akipata uchungu wa kujifungua, gari la wagonjwa linamfuata nyumbani na kumpleka hospitali, hii yote ni nia dhabiti ya Mhe. Rais ya kupunguza na hatimaye kuondoa kabisa vifo vyabkina Mama wanaoenda kujifungua.
Programu ya Uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi na Mama Samia (IMASA) inatekelezwa kuanzia katika ngazi ya vitongoji, mitaa, vijiji hadi ngazi ya Taifa.