Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi limeendesha semina ya siku tatu kuanzia tarehe 15 hadi 17Mkoani Mwanza kwa watoa huduma wa maendeleo ya biashara nchini (BDSPs). Semina hiyo imelenga kukusanya maoni yanayolenga kuboresha rasimu ya mwongozo wa kitaifa wa uanzishaji na usimamizi wa vituo vya uendelezaji wa wajasiriamali na kujenga uwezo wa watoa huduma juu ya Urasimishaji wa biashara.
Mafunzo hayo yamelenga watoa huduma wa Mkoa wa Mwanza, Shinyanga na Geita. Programu hii ni uendelezaji wa jitihada za Baraza katika kuchochea maendeleo ya ujasiriamali nchini na kuwawezesha watanzania kuweza kunufaika na fursa zinazopatikana katika sekta ya uziduaji kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) kwa ufadhili wa benki ya maendeleo ya Afrika (TADB).