BARAZA LA TAIFA LA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI LAFANYA KIKAO CHA MAZINGATIVU MIKUMI MKOANI MOROGORO.
Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi limefanya kikao cha Mazingativu Mikumi Mkoani Morogoro.
Kikao hicho kimeongozwa na Katibu Mtendaji wa Baraza Bibi Beng'i Issa na watumishi wote wa Baraza.
Sambamba na hilo Katibu Mtendaji alitoa wasilisho la stadi za maisha kwa watumishi.
Vile vile watumishi walipata fursa ya kupata wasilisho kutoka kwa Afisa wa Benki Kuu Bw. Hussein Masoud kuhusu masuala mazima ya Uwekezaji. Utunzaji wa fedha na namna bora ya kustaafu.
Katibu Mtendaji aliwashukuru watumishi wote kwa ushirikiano walioutoa na kuwaomba kuzingatia zaidi suala la muda.
Kikao hicho kitaendelea kwa siku tatu na kinatarajia kufikia tamati tarehe 30 kwa watumishi wote kutembelea mbuga za wanyama.