Majukumu ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ni yapi?
1. Kuendesha na Kusimamia mashauri yote ya Madai, Haki za Binadamu,Kikatiba na Usuluhishi zinazoihusu Serikali;
2. Kutoa miongozo kwa Wanasheria na Mawakili wa Serikali ambao wanasimamia uendeshaji wa kesi za madai, kesi za haki za binadamu, na Kikatiba na mashauri ya usuluhishi yanayoihusu Serikali;
3. Kuratibu Mashauri ya Madai, Haki za Binadamu, kesi za Kikatibana Usuluhishi katika Mahakama na Mabaraza ya Usuluhishi kwaniaba ya Serikali;
4. Kuandaa na kufungua mashauri ya madai ikiwemo Katiba, Hakiza Binadamu na Usuluhishi kwenye Mahakama na Mabaraza ya Usuluhishi ndani na nje ya Tanzania;
5. Kutoa ushauri wa Serikali kuhusu mashauri ya Madai na Usuluhishi na Kuratibu mwenendo wa mashauri ya Serikaliyaliyopo Mahakamani na Mabaraza ya Usuluhishi ndani na nje ya nchi;
6. Kuchukua jukumu la kuendesha mashauri au kesi yeyote yenye maslahi umma; na
7. Kutunza kukbukumbu za mashauri au kesi zote za Serikali na kutoa taarifa mara kwa mara wadau husika.