Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali

Menejimenti ya OWMS yatakiwa kuongeza ushirikiano katika kutekeleza majukumu yake.

Imewekwa: 25 October, 2024
Menejimenti ya OWMS yatakiwa kuongeza ushirikiano katika kutekeleza majukumu yake.

Wajumbe wa Menejimenti ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kutekeleza majukumu yao kwa kushirikiana hatua itakayowasaidia kutekeleza majukumu yao kwa wakati ili kufikia malengo yao waliyojiwekea ndani ya muda ulipangwa.

Wito huo umetolewa na Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Ally Possi wakati wa kikao cha kwanza cha Menejimenti tangu alipoteuliwa kushika nafasi hiyo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kilicholenga kufahamiana na kutoa mwelekeo wa utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku kilichofanyia kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi hiyo Jijini Dar es Salaam.

Ameongeza kuwa kufanya kazi kwa ushirikiano kutawasaidia viongozi hao kuwa na mtazamo wa pamoja katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku hasa jukumu mama la kusimamia, kuratibu na kuendeshamashauri yote ya madai na usuhishi yaliyopo katika mahakama mbalimbali chinini na hatmaye kuisaidia ofisi hii kupata ushindi mara mashauri hayo yanapomalizika.

Kiongozi huyo ameeleza kuwa Kufanya kazi kwa ushirikiano ni muhimu kwa kuwa kutawasaidia viongozi wa ofisi hiyo kuongeza ujuzi, uzoefu, na kuwa na mitazamo chanya ya pamoja na kuongeza  ubunifu utakao saidia kupata suluhisho sahihi katika kukabiliana na Changamoto zilizopo.

Katika hatua nyingine Dkt. Possi amewataka viongozi hao kutekeleza majuku yao kwa ufanisi ikiwa ni pamoja na kuwa wepesi wa kutoa ushauri wenye tija ili kwa pamoja kama viongozi waweze kusaidia kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.

Aidha, amewsihi viongozi hao kuendelea kuwasimamia vyema watumishi walioko chini yao ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabiri sambasamba na kujali maslahi yao ya kuitumishi ili watumishi hao waweze kutekeleza kutekeleza majukumu yao kwa wakati.

Kiongozi huyo pia amewasisitiza wajumbe wa menejimenti ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kuendelea kutekeleza majukumu yako kwa kufuata Sheria, taratibu na kanuni za kudumu za utumishi wa umma kwa kuwa Kufanya kazi kwa kufuata sheria, taratibu, na kanuni za utumishi wa umma ni msingi wa utoaji wa huduma bora kwa wananchi na kuhakikisha kwamba utumishi wa umma unafanyika kwa njia ya uwazi, uadilifu, na uwajibikaji wakati wote wawapo ndani na nje ya kituo cha kazi.

Naye, Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Bi. Alice Mtulo akizungumza na wajumbe hao wakati akisoma taarifa ya utekelezaji ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ameahidi kumpa ushirikiao kiongozi huyo pamoja na kufanyia kazi maelekezo na miongozo yote atakayoitoa kwa lengo la kuhakikisha wanamsaidia Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwaletea wananchi Maendeleo.