The United Republic of Tanzania

Public Private Partnership Centre

( PPPC )

Njia nne (4) ambazo Serikali na Sekta Binafsi wanaweza kuingia ubia

Posted On: 24 August, 2024
Njia nne (4) ambazo Serikali na Sekta Binafsi wanaweza kuingia ubia

"Kuna njia kama nne ambazo Serikali na Sekta binafsi wanaweza kuingia ubia
1. Mradi wenye sifa za kibiashara ambapo Serikali inatoa zabuni inaruhusu wawekezaji binafsi kuleta andiko na atakaekuwa na andiko zuri basi anapata nafasi.
2. Sekta binafsi inaona jinsi serikali inafanya jambo inafanya kwa hasara ila ukifanya wewe unaweza kufanya kwa faida. Huitaji kusubiri zabuni ila unaandika wewe andiko
3. Makubaliano ya moja kwa moja kwamba serikali inahitaji mradi kwa haraka hivyo mchakato ukienda kawaida itachukua muda hivyo mamlaka husika inaruhusiwa kutafuta sekta binafsi na kuongea nao moja kwa moja ili mradi uweze kukamilika kwa wakati
4. Special arrangement. Makubaliano maalumu ambayo yanatokea pale ambapo sheria imewekwa lakini kuna vitu havikutazamwa hivyo kuna miradi itakwama ndipo wanakaa na kuuzungumzia tena. Hii inaonyesha utayari wa Serikali kufanya kazi na sekta binafsi" - Mkurugenzi wa kituo cha ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi (PPPC) Bw. David Kafulila