Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania

"Mionzi kwa Matumizi Salama na Teknolojia ya Nyuklia kwa Maendeleo ya Taifa"
Nyumbani / Habari / Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omary Juma Kipanga aweka Jiwe lamsingi, Ujenzi wa Maabara na Ofisi ya Kanda ya TAEC, Mwanza

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omary Juma Kipanga aweka Jiwe lamsingi, Ujenzi wa Maabara na Ofisi ya Kanda ya TAEC, Mwanza

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omary Juma Kipanga aweka Jiwe lamsingi, Ujenzi wa Maabara na Ofisi ya Kanda ya TAEC, Mwanza

Published on December 22, 2021

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omary Juma Kipanga (Mb) ameipongeza Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) kwa Maendeleo Mazuri ya mradi wa Ujenzi wa Ofisi na Maabara ya kanda inayoendelea kujengwa Jijini Mwanza.

Mhe. Naibu Waziri ameyasema hayo Jijini Mwanza alipokuwa akiweka Jiwe la msingi la ujenzi wa Maabara ya TAEC eneo la Nyegezi siku ya Jumanne tarehe 14/12/2021 ambapo amewaambia wananchi waliohudhuria halfa hiyo kuwa jukumu la Serikali ni kuhakikisha kwamba huduma zinasogezwa kwa wananchi, hivyo basi uwepo wa Maabara hiyo utasaidia kuimarisha huduma za udhibiti wa matumizi salama ya Mionzi kwa wananchi wa Kanda ya Ziwa na hatimae kulinda afya zao dhidi ya madhara yanayoweza kusababishwa naMionzi.

Awali, akitoa taarifa ya mradi wa ujenzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania, Prof. Lazaro Busagala ameishukuru serikali kwa kuendelea kutenga fedha kwa ajiri ya miradi mbalimbali itakayosaidia upatikanaji wa huduma za kinga ya mionzi kwa wakati. Aidha, Mkurugenzi Mkuu aliwaeleza wananchi waliohudhuria hafla hiyo kuwa, huduma za Tume kwa sasa zinapatikana kwa muda mfupi zaidi tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

“Kwa sasa vibali vya mionzi vinatolewa ndani ya muda mchache na kwa muda usiozidi siku moja kibali kinapatikana tofauti na ilivyokuwa awali ambapo ilikuwa ikichukua hadi muda wa siku saba ili mteja kupata kibali”

Maabara hii ya kanda inajengwa na Serikali kwa gharama ya shilingi Bilioni 2.8 ambapo jumla ya mikoa nane (8) ya Kanda ya Ziwa itakuwa ikipata huduma kupitia Maabara hii.

Ni juhudi nyingine ya Serikali katika kufikisha huduma kwa wananchi na kuwawezesha wafanyabiashara kupata vibali vya Mionzi kwa wakati hivyo kuharakisha na kuwezesha Biashara