Historia
Published on January 20, 2025
Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (pia inajulikana kwa kifupi kama TAEC) ni chombo cha udhibiti kinachohusika na masuala yote ya nguvu za Atomu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ilianzishwa chini ya Sheria ya Nguvu za Atomu Namba 7 ya mwaka 2003. Uundwaji wa TAEC mwaka 2003 ulianza kutekelezwa baada ya kufutwa kwa Sheria ya Kinga ya Mionzi Namba 5 ya mwaka 1983, ambayo iliunda Tume ya Taifa ya Mionzi (NRC) mwaka 1983. TAEC iliundwa ikiwa na majukumu ya ziada, ikiwemo kudhibiti matumizi ya vyanzo vya mionzi ayonishi na isiyo ayonisha, pamoja na kukuza matumizi salama na ya amani ya nguvu za atomu na teknolojia ya nyuklia. Vilevile, TAEC inadhibiti matumizi salama na ya amani ya nguvu za atomu na kukuza na kupanua mchango wa nguvu za atomu na teknolojia ya nyuklia katika afya na ustawi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.