Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania

"Mionzi kwa Matumizi Salama na Teknolojia ya Nyuklia kwa Maendeleo ya Taifa"
Nyumbani / Habari / TAEC na IAEA Imeendesha Kozi ya Kikanda ya Mafunzo Kuhusu Uchambuzi wa Mahitaji ya Nishati

TAEC na IAEA Imeendesha Kozi ya Kikanda ya Mafunzo Kuhusu Uchambuzi wa Mahitaji ya Nishati

TAEC na IAEA Imeendesha Kozi ya Kikanda ya Mafunzo Kuhusu Uchambuzi wa Mahitaji ya Nishati

Published on September 13, 2024

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Profesa Daniel Mushi leo Septemba 10, 2024 afungua rasmi kozi ya Kikanda  ya mafunzo kuhusu Uchambuzi wa Mahitaji ya Nishati kulingana na utumiaji wa Muundo wa Uchambuzi wa Mahitaji ya Nishati wa IAEA (MAED).

Mafunzo haya yaliyoanza rasmi jana tarehe 09 Septemba 2024 katika hoteli ya Corridor Spring ya Jijini Arusha  yanaratibiwa na Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) kwa kushirikiana na Shirika la Nguvu za Atomu Duniani (IAEA) na Shirika la Umeme la Afrika Mashariki (EAPP)

Kozi ya mafunzo inalenga kuongeza uwezo wa mahitaji ya nishati kwa wanasayansi, wapangaji mipango na watoa maamuzi katika nchi za ukanda wa nishati wa Africa Mashariki.

 Malengo makuu ni kuwapa ufahamu na kuwawezesha washiriki matumizi ya MAED kwa uchanganuzi wa mahitaji ya nishati, kusaidia mikakati ya nishati ya kitaifa na kikanda kwa maendeleo endelevu ya nishati na kuwezesha maamuzi yanayotokana na data katika sera ya nishati na ugawaji wa rasilimali.

 Mafunzo yamejumuisha washiriki 50 kutoka nchi wanachama wa EAPP ambazo ni: Misri, Sudan, Sudan Kusini, Djibouti, Somalia, Ethiopia, Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kenya, Burundi, Rwanda na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 Mafunzo haya yatawapa washiriki ujuzi wa vitendo katika utabiri na uchambuzi wa mahitaji ya nishati kwa kutumia zana ya MAED. Mazingatio zaidi yamelenga  katika kuchanganua mahitaji ya nishati kwa kusisitiza upangaji na sera za nishati, mambo ya kiuchumi ya kijamii yanayoathiri mahitaji ya nishati kwa kutabiri mahitaji ya nishati ya siku zijazo.

 Kozi hiyo itaendeshwa kwa wiki mbili ikijumuisha mafunzo ya vitendo, masomo ya kifani, na mazoezi shirikishi ili kuhakikisha kuwa washiriki wanaweza kutumia maarifa na ujuzi waliopata kwenye matukio ya ulimwengu halisi katika nchi zao. Mafunzo hayo yatafungwa Ijumaa, tarehe 20 Septemba,  2024.