Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania

"Mionzi kwa Matumizi Salama na Teknolojia ya Nyuklia kwa Maendeleo ya Taifa"
Nyumbani / Habari / TAEC imeshiriki maonesho viwanja vya Nyamazi Unguja kuadhimisha kilele cha Miaka 61, ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ili kuendelea kutoa elimu kwa umma

TAEC imeshiriki maonesho viwanja vya Nyamazi Unguja kuadhimisha kilele cha Miaka 61, ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ili kuendelea kutoa elimu kwa umma

TAEC imeshiriki maonesho viwanja vya Nyamazi Unguja kuadhimisha kilele cha Miaka 61, ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ili kuendelea kutoa elimu kwa umma

Published on January 20, 2025

Article cover image

Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) imeendelea kushiriki kikamilifu maonesho ya elimu na  biashara  yanayoendelea kufanyika viwanja vya  nyamazi Unguja ili kuendelea kutoa elimu kwa umma juu ya udhibiti wa matumizi salama ya mionzi pamoja na uhamasishaji wa matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia nchini katika seka za afya, kilimo, mifugo,maji, nishati, viwanda, migodi nk.

Kitaifa kwa mwaka huu maadhimisho ya maonesho hayo yamefanyikia katika uwanja wa Gombani, wilaya ya Chakechake, mkoa wa Kusini Pemba, Zanzibar ambapo kilele chake kilikuwa jana tarehe 12 Januari, 2025.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alishiriki katika kilele hicho cha   Miaka 61, ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na  Mgeni Rasmi wa maadhimisho hayo alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi

TAEC hushiriki maonesho haya kila mwaka ili kuendelea kutoa elimu juu ya majukumu na kazi zake inazotekeleza kisheria ili kukuza uelewa kwa wananchi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Maonesho haya uandaliwa maalumu kila mwaka katika kuadhimisha sikukuu ya Mapinduzi ambapo kwa mwaka huu Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) inaadhimisha miaka 61 tangu ilipotokea mapinduzi hayo mwaka 1964.

TAEC imekuwa ikitumia nafasi hii muhimu ya kushiriki maadhimisho ya maonesho ya mapinduzi matukufu ili kusikiliza na kujibu changamoto za wafanyabiashara pamoja na kuelezea utaratibu mzima wa utolewaji wa vibali vya mionzi wakati wa uingizaji na usafirishaji wa bidhaa nje ya nchi.

Maonesho haya ya  siku kumi na tano (15) yalianza rasmi tarehe 01 Januari, 2025 na kilele chake ni tarehe 15 Januari, 2025. Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) ndio iliyoratibu maonesho haya ikishirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).