Monthly Forecast
Monthly Forecast
MWELEKEO WA HALI YA HEWA KWA MWEZI OKTOBA, 2025
Katika kipindi cha mwezi Oktoba 2025, mvua za msimu wa Vuli zinatarajiwa kuanza katika maeneo mengi yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka. Aidha, mvua za chini ya wastani hadi wastani pamoja na mtawanyiko hafifu zinatarajiwa katika maeneo mengi. Kwa upande mwingine, hali ya joto kiasi hadi joto kali inatarajiwa hususan katika maeneo yanayotarajiwa kupata vipindi vichache vya mvua. Vipindi vya upepo mkali vinatarajiwa kujitokeza hususan katika maeneo ya ukanda wa pwani na maziwa makuu.

