24 Forecast
24 Forecast
UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO 26.10.2025
Vipindi vifupi vya mvua kubwa vinatarajiwa katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Dar es salaam, Morogoro, Tanga na Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia) pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba. Aidha, vipindi vifupi vya upepo mkali unaofikia Kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita 2 vinatarajiwa katika baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani mwa Bahari ya Hindi.

