Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

ISO 9001:2015 Imethibitishwa Kutoa Huduma za Hali ya Hewa kwenye Usafiri wa Anga

10 Days Forecast

Utabiri wa Siku 10

MWELEKEO WA MVUA KWA TAREHE 01-10 DESEMBA, 2025

Kanda ya ziwa Victoria (Mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Mwanza, Simiyu na Mara): Vipindi vya mvua zinazoambatana na ngurumo za radi vinatarajiwa katika maeneo machache hususan katika kipindi cha siku tano za mwisho.

Nyanda za juu kaskazini-mashariki (Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro): Hali ya ukavu kwa ujumla inatarajiwa.

Pwani ya kaskazini (Mikoa ya Tanga, Maeneo ya kaskazini mwa Morogoro, Pwani na Dar es Salaampamoja na visiwa vya Unguja na Pemba): Vipindi vyamvua nyepesi vinatarajiwa katika maeneo machache hususan katika kipindi cha siku tano za mwisho.

Magharibi mwa nchi (Mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabora): Mvua zinazoambatana na ngurumo za radi zinatarajiwa katika maeneo machache ya mikoa ya Kigoma na Katavi hususan katika kipindi cha siku tano za mwisho.

Kanda ya kati (Mikoa ya Dodoma na Singida): Hali ya ukavu kwa ujumla inatarajiwa.

Nyanda za juu Kusini-magharibi (Mikoa ya Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Iringa): Vipindi vya mvua vinatarajiwa katika maeneo machache hususan katika kipindi cha siku tano za mwisho.

Pwani ya kusini (Mikoa ya Mtwara na Lindi): Vipindi vya mvua nyepesi vinatarajiwa katika maeneo machache hususan katika kipindi cha siku tano za mwisho.

Kanda ya kusini (Mkoa wa Ruvuma na Maeneo ya kusini mwa Morogoro):Vipindi vya mvua vinatarajiwa katika maeneo machache hususan katika kipindi cha siku tano za mwisho.

Imetolewa na:

MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

Kwa maelezo zaidi tafadhali PAKUA