20 May, 2024 8:30AM-2:00PM JNICC - Dar es Salaam

Kaimu Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania anapenda kuwatangazia wahitimu wote na wadau wa Chuo cha Utumishi wa Umma kwa ujumla kuwa Mahafali ya Thelathini na Tisa (39) kwa Kampasi zote za Chuo yatafanyika   siku ya Alhamisi , tarehe 6 Juni  2024 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Dar es Salaam, kuanzia saa tatu (03.00) asubuhi.

Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango

Aidha, wahitimu wote wanahimizwa kuhudhuria mahafali hayo. Mazoezi (Rehearsal) yatafanyika siku ya Alhamisi tarehe 5 Juni 2024 Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere kuanzia saa nane (08.00) mchana.

 Wahitimu wanatakiwa kuvaa suti zinazokubalika Chuoni (rangi nyeusi au dark blue) na majoho rasmi ya wahitimu. Gharama ya Joho ni shilingi 10,000/= kwa wahitimu wote.

Aidha, wahitimu mnatakiwa kuthibitisha ushiriki wenu kupitia namba. 0713577587/0715092197

MAHAFALI YA 39 YA CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA TANZANIA
Feedbacks

Mrejesho, Malalamiko au Wazo