Dira

Kuwa kituo cha mafunzo chenye uwezo wa hali ya juu katika kuendeleza utendaji uliotukuka katika utumishi wa Umma.
Kwa kutumia Dira hii, Chuo kitachangia katika maendeleo ya utumishi wa umma, unaolenga matokeo ambayo ni kuwatumikia Watanzania kwa umadhubuti na ufanisi mkubwa.

Dhamira

“Kukuza kiwango cha ubora, utendaji na ufanisi wa huduma za Utumishi wa Umma Tanzania kwa kutoa mafunzo muafaka, ushauri wa kitaalamu, na kujikita katika tafiti mbalimbali”

Maadili Yetu

  • Kuthamini Mteja: Tutatoa huduma bora ili kukidhi mahitaji na matarajio ya wadau.
  • Uadilifu: Tunazingatia viwango vya juu zaidi vya kimaadili, uaminifu na kuzingatia Utawala Bora katika kutekeleza majukumu.
  • Ubunifu: Tunadumisha ubunifu endelevu katika matumizi ya technolojia zinazofaa ili kukuza na kutoa huduma bora.
  • Weledi: Tunazingatia kiwango cha juu cha umahili na viwango bora katika kutekeleza majukumu ili kukidhi mahitaji na matarajio ya wadau.
  • Kutoa Huduma bila upendeleo: Tunazingatia usawa na kuepuka ubaguzi wa aina yoyote ya upendeleo katika utoaji wa huduma.
  • Ushirikiano katika Kazi: Tunajenga na kuhimiza uhusiano wa kikaziwa kirafiki na shirikishi miongoni mwawatumishi katika kufikia malengo ya kitaasisi.
Feedbacks

Mrejesho, Malalamiko au Wazo