Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) ulianzishwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Sheria ya Bunge nambari 11 ya mwaka 2006 Sura ya 422 kwa lengo la kupeleka na kufanikisha huduma ya mawasiliano kwa wananchi waishio katika maeneo machache ya mijini na maeneo mengi yaliyo mbali vijijini yasio na mvuto wa kibiashara kwa watoa huduma ya mawasiliano. Mwaka 2009 kanuni za kuhuisha Mfuko zilipitishwa na Mfuko kuanza kazi tarehe 1 Julai 2009.