Royal, International and Master Health Check up Clinic

July 16, 2025
Royal, International and Master Health Check up Clinic image

Huduma za Wateja Maalum, Wagonjwa wa Kimataifa na Uchunguzi wa Kina wa Afya

 

Huduma za Wateteja Malum na Uchunguzi wa Kina wa Afya

Huduma zetu za Wateja maalum zinawahudumia watu mashuhuri wa hadhi ya juu na wagonjwa binafsi wanaopatiwa huduma katika vyumba vya binafsi wakiwa na madaktari bingwa na wauguzi maalumu waliowekwa kwa ajili yao. Wagonjwa hupata huduma kwa haraka katika mashauriano, uchunguzi na matibabu. Pia wanaweza kupanga miadi ya haraka, upasuaji na vipimo, kufurahia muda mfupi wa kusubiri na kupewa njia za kuingia na kutoka binafsi.

 

Kliniki ya Wagonjwa Wa Kimataifa

Kliniki ya Wagonjwa wa Kimataifa (IPC) inatoa huduma za matibabu na msaada kwa watu wanaosafiri kutoka nje ya nchi kuja kupokea huduma za afya. Tunatoa huduma maalumu, msaada wa lugha na ushauri wa mipango ya kifedha ili kurahisisha mchakato kwa wagonjwa wa kimataifa. Wasiliana nasi kupitia +255 767 652 201.

 

Uchunguzi Wa Kina Wa Afya

Tunatoa uchunguzi wa kina wa kiafya unaolenga kutathmini afya ya jumla ya mtu na kubaini matatizo au hatari za kiafya mapema, hata kabla dalili hazijaonekana. Kwa kutambua vihatarishi mapema, uchunguzi wa afya wa kina (master health check-up) unasaidia kuchukua hatua za haraka na kufanya mabadiliko ya mtindo wa maisha, jambo linaloweza kuzuia magonjwa makubwa zaidi siku za usoni. Unaweza kuwasiliana nasi kwa urahisi kupitia namba ya simu +255 735 000 002.

 

Faida za ziada kwa huduma zote zilizotajwa;

  • Huduma za ubingwa wa hali ya juu na mashauriano ya kitaalamu mbalimbali
  • Upasuaji siku hiyo hiyo

  • Huduma za uchunguzi wa haraka (Maabara na X-ray, Ultrasound, CT scan na MRI)

  • Ushauri wa daktari ndani ya dakika 10 baada ya kuwasili

  • Huduma za duka la dawa saa 24

  • Huduma za gari la wagonjwa saa 24

  • Chumba cha mapumziko cha viongozi (Executive Lounge)

  • Uongozaji kuanzia lango la kuingilia

  • Vinywaji (Maji safi, Kahawa, Chai na Juisi)

  • Malazi nafuu kwa wagonjwa wa kimataifa

  • Muda mfupi wa kupata majibu (TAT)

  • Wi-Fi ya bure