Afya ya Mtoto
Published on August 14, 2022
IDARA YA TIBA NA AFYA YA MTOTO
HUDUMA ZITOLEWAZO
Tunafanya Uchunguzi, Matibabu na Ushauri kwa watoto na vijana wa umri wa miaka 0-14.
1. Baadhi ya huduma za UCHUNGUZI.
Tunafanya uchunguzi wa magonjwa mbalimbali yanayoathiri Afya ya Mtoto;
- Afya ya Lishe
- Uchunguzi wa Magonjwa yanayoathiri Mfumo wa hewa
- Uchunguzi wa Magonjwa yanayoathiri Damu na Saratani kwa watoto
- Uchunguzi wa Magonjwa yanayoathiri Moyo
- Uchunguzi wa Magonjwa yanayoathiri Afya ya akili
- Baadhi za huduma za MATIBABU
- Matibabu ya watoto wenye magonjwa ya Moyo
- Matibabu ya Magonjwa yanayoathiri Mfumo wa Chakula
- Magonjwa yanaathiri watotoNjiti na waliyopata shida kutokana na changamoto za uzazi.
- Matibabu ya maginjwa yahusuyo mfumo wa damu na saratani.
- Tiba na Huduma wezeshi kwa watoto wenye mtindio wa Ubongo na Kifafa.
- Ufuatiliaji wa makuzi na ya mtoto kuanzia anapozaliwa mpaka anapofikia umri wa barehe.
Idara ya Afya ya Watoto ya Hospitali ya Benjamin Mkapa inao madaktari Bingwa na Bingwa bobezi na wataamu wenye uwezo wa kumhudumia mtoto kwa viwango vya juu vya ubora kwa ngazi za kimataifa.