Mwanzo / Kurasa / Upasuaji wa Moyo

Upasuaji wa Moyo

Upasuaji wa Moyo

Published on August 13, 2022

VIPIMO

Madaktari pia watachukua  historia ya mgonjwa  ili kubaini magonjwa na matibabu aliyopata kipindi cha nyuma  ikiwepo  dalili  alizokuwa nazo.

Mgonjwa hufanyiwa vipimo kadha wa kadha vya maabara,kubanini sababu au vitu vinavyoongeza tatizo la kuwa na mapigo chini ya kiwango.

Vipimo vya moyo

ECG -ili kuangalia mfumo wa umeme na hasa mapigo ya moyo yako kwa kiwango gani kipimo ECHO-kubaini kama kuna shida kwenye moyo ambayo inaweza kuwa sababishi.

Vipimo vingine anavyopitia mtu mwenye mapigo ya chini ya kiwango cha 40 zinazoambatana na dalili ni Holter ECG pamoja na Stress ECG. Vipimo vyote hivi vinapatikana Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma

CHANZO

Umri unaweza kuwa mojawapo ya chanzo cha mapigo kuwa chini ya kiwango cha 40. Wazee wanaweza kupata tatizo hili

Baadhi ya maradhi ya moyo yanaweza kuwa sababu ya mapigo ya moyo kuwa chini ya kiwango cha 40

Matibabu yanayotumika kutibu shinikizo juu la damu na magonjwa mengine ya moyo  ikiwemo ya mfumo wa umeme.( DAWA)

Upasuaji wa moyo unaweza kuwa sababu ya mapigo ya moyo chini ya kiwango cha 40,upasuaji huweza kuathiri mfumo wa umeme

BAADA YA KUPANDIKIZWA BETRI

Baada ya kupandikizwa betri kwenye moyo, mtu atapaswa aishi maisha ya tahadhari ikiwa ni pamoja na matumizi ya simu.

Mtu atapaswa aiweke mbali kama nchi sita anapo pokea simu ili kuepusha mawimbi kuhitalifiana na betri aliyopandikizwa.

Mwenye betri kwenye moyo pia hatopaswa kupita kwenye ving’amuzi chuma (metal detectors) sababu inaweza kuhitalifiana na betri hilo.

Atapaswa kuepuka matumizi ya sigara za kielectroniki (e-cigarette) na mazoezi ya nguvu. Pia aepuke vifaa vya umeme ambavyo vina hitilafu kama micro wave na blanketi ya kielectroniki.

 

UMRI WA BETRI

Baada ya kupandikizwa betri, mtu anaweza kudumu na betri moyoni kwa muda wa muda wa miaka sita mpaka kumi na mbili kabla ya haijabilishwa tena.