Nyurolojia na Mifupa
Published on August 12, 2022
Idara ya Mifupa na Mishipa ya fahamu, ilianza kutoa huduma Novemba 2017, ikiwa na watoa huduma wanne, Daktari bingwa wa upasuaji mifupa, na Wauguzi watatu.
Idara ya Mifupa na Mishipa ya fahamu, ilianza kwa kutoa huduma za Upasuaji wa Mifupa (Trauma), kuona Wagonjwa wa nje na wa ndani (in and out patient), ambapo wagonjwa 30 walionwa na kupatiwa huduma kila siku.
Idara ya Mifupa na Mishipa ya fahamu, katika ya 2018 hadi January 2022, idara hii imeongeza huduma mbalimbali, ikiwa ni pamoja na; Upasuaji wa kubadili Nyonga na Magoti, Upasuaji wa Matundu (arthroscopy).
Idara ya Mifupa na Mishipa ya fahamu, kwa sasa imeongeza uwezo wake wa Rasilimali watu, ambapo Madaktari bingwa wa Upasuaji wa mifupa wamefikia 5, huku Madaktari wa kawaida(registrar) wakifikia 6.
Kwa wastani, Idara ya Mifupa na Mishipa ya fahamu, huona wagonjwa 100 kwa siku na hufanya upasuji kwa wagonjwa 25 kwa wiki.
IDARA YA UPASUAJI WA UBONGO, MISHIPA YA FAHAMU, UTI WA MGONGO
Idara ya Upasuaji wa Ubongo, Mishipa ya Fahamu, Uti wa Mgongo ilianzishwa July 2022 ikiwa na idadi ya watendaji wanne, ambao ni Daktari Bingwa mmoja, Madaktari wawili na Muuguzi mmoja wa Kiliniki ya Nje.
Idara ilianza kwa kutoa huduma ya kuona wagonjwa wa nje (outpatient clinic) pamoja na Upasuaji wa Dharura wa Ubongo na Uti wa Mgongo.
Agosti 2020, Idara ya Upasuaji wa Ubongo, Mishipa ya Fahamu, Uti wa Mgongo iliongeza huduma kwa kuanza kufanya Upasuaji wa Kupangiwa (elective surgery) kwa wagonjwa waliyohitaji huduma za upasuaji katika Ubongo na Uti wa mgongo.
Septemba 2020, Idara ya Upasuaji wa Ubongo, Mishipa ya Fahamu, Uti wa Mgongo ilipatiwa Chumba cha Upasuaji maalumu kwa Uti wa Mgongo na Mishipa ya fahamu.
Hivyo, ikaongeza huduma mbalimbali kama vile; Upasuaji Mkubwa wa Kibingwa wa kutoa vimbe katika Ubongo na Uti wa mgongo, Upasuaji wa Mgongo kwa waliyovunjika kwa kutumia vipandikizi vya kuunga.
Juni 2021, Idara ya Upasuaji wa Ubongo, Mishipa ya Fahamu, Uti wa Mgongo ilianzisha huduma upasuaji wa matatizo ya Ubongo kwa kutumia kamera inayopita kwenye matundu madogo (endoscopic surgery) mfano, kwa watoto wenye vichwa vikubwa, na vimbe katika ubongo.
Kliniki inayoendeshwa na Idara ya Upasuaji wa Ubongo, Mishipa ya Fahamu, Uti wa Mgongo ilianza kwa kuona wagonjwa 10 kwa siku, kwa sasa ina wastani wagonjwa 30 kila siku.
Hadi Januari 2022, Idara ya Upasuaji wa Ubongo, Mishipa ya Fahamu, Uti wa Mgongo inamadaktari Bigwa 2, Madktari 3, Wauguzi 3, na tangu ilipoanzishwa, idara hiyo imehudumia wagonjwa wapatao, 8347.