Mwanzo / Huduma Zetu / Waliopandikizwa betri kwenye moyo BMH wafikia 8.

Waliopandikizwa betri kwenye moyo BMH wafikia 8.

Waliopandikizwa betri kwenye moyo BMH wafikia 8.

Published on August 12, 2022

Article cover image

Na Ludovick Kazoka

WATU takribani 8 waliokuwa na matatizo ya mapigo ya moyo wamepandikizwa betri kwenye moyo mpaka kufikia mwezi Mei katika Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) toka huduma ilipoanzishwa mwaka uliopita.

Upandikizaji wa betri kwenye moyo ni upandikizaji wa kifaa cha kieletroniki kwenye moyo kwa watu wenye tatizo la mapigo ya moyo ya chini. Upandikizaji wa betri kwenye moyo upo wa aina mbili wa kudumu na usio wa kudumu.

Mkuu wa Idara ya Matibabu ya Magonjwa ya Moyo, Dkt Happiness Kusima, ameliambia jarida hili kuwa mapigo ya moyo ya kawaida ni kuanzia 60 mpaka 100 kwa mtu mwenye umri wa zaidi ya miaka 12 na wengi wanaohitaji upandikizaji huo ni walio na mapigo chini ya 40 yanayoambatana na dalili.

“Mpaka sasa, tumepandikiza betri kwa watu wawili  waliokuwa na tatizo la mapigo ya moyo ya chini, mmoja tulimpandikiza tarehe 1 na wa pili tarehe 28 mwezi Oktoba mwaka huu 2021” alisema Mkuu wa Idara ya Matibabu ya Moyo katika BMH.

Watu gani wanapandikizwa betri kwenye moyo

Kwa mujibu wa Dkt Kusima, watu wenye mapigo ya moyo chini ya kiwango cha 40 yanayoambatana na dalili wanapandikizwa betri kwenye moyo baada ya kupitia vipimo kadhaa vya moyo

Pia, anasema kuwa baadhi ya watu wenye tatizo la kushindwa kwa moyo (heart failure) ambao baada ya uchunguzi kuonekana wana hitilafu kwenye mfumo wa umeme wanapandikizwa betri kwenye moyo.

Dalili za watu wenye tatizo la mapigo ya moyo chini ya kiwango cha 40

  • Uchovu wa hali ya juu
  • Kupoteza fahamu
  • kupata shida ya kupumua.
  • Kizunguzungu
  • Maumivu kwenye kifua

 

Hata hivyo, Dkt Kusima, anasema sio kila mtu mwenye mapigo chini ya kiwango cha 40 anapaswa kupandikizwa betri kwenye moyo, akisema mapigo ya moyo chini ya 40 ndiyo yakiambatana na dalili hizo ndiyo anafanyiwa vipimo kuangalia uwezekano wa kumpandikizia betri.

VIPIMO

Madaktari pia watachukua  historia ya mgonjwa  ili kubaini magonjwa na matibabu aliyopata kipindi cha nyuma  ikiwepo  dalili  alizokuwa nazo.

Mgonjwa hufanyiwa vipimo kadha wa kadha vya maabara,kubanini sababu au vitu vinavyoongeza tatizo la kuwa na mapigo chini ya kiwango.

Vipimo vya moyo

ECG -ili kuangalia mfumo wa umeme na hasa mapigo ya moyo yako kwa kiwango gani kipimo ECHO-kubaini kama kuna shida kwenye moyo ambayo inaweza kuwa sababishi.

Vipimo vingine anavyopitia mtu mwenye mapigo ya chini ya kiwango cha 40 zinazoambatana na dalili ni Holter ECG pamoja na Stress ECG. Vipimo vyote hivi vinapatikana Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma

CHANZO

Umri unaweza kuwa mojawapo ya chanzo cha mapigo kuwa chini ya kiwango cha 40. Wazee wanaweza kupata tatizo hili

Baadhi ya maradhi ya moyo yanaweza kuwa sababu ya mapigo ya moyo kuwa chini ya kiwango cha 40

Matibabu yanayotumika kutibu shinikizo juu la damu na magonjwa mengine ya moyo  ikiwemo ya mfumo wa umeme.( DAWA)

Upasuaji wa moyo unaweza kuwa sababu ya mapigo ya moyo chini ya kiwango cha 40,upasuaji huweza kuathiri mfumo wa umeme

BAADA YA KUPANDIKIZWA BETRI

Baada ya kupandikizwa betri kwenye moyo, mtu atapaswa aishi maisha ya tahadhari ikiwa ni pamoja na matumizi ya simu.

Mtu atapaswa aiweke mbali kama nchi sita anapo pokea simu ili kuepusha mawimbi kuhitalifiana na betri aliyopandikizwa.

Mwenye betri kwenye moyo pia hatopaswa kupita kwenye ving’amuzi chuma (metal detectors) sababu inaweza kuhitalifiana na betri hilo.

Atapaswa kuepuka matumizi ya sigara za kielectroniki (e-cigarette) na mazoezi ya nguvu. Pia aepuke vifaa vya umeme ambavyo vina hitilafu kama micro wave na blanketi ya kielectroniki.

 

UMRI WA BETRI

Baada ya kupandikizwa betri, mtu anaweza kudumu na betri moyoni kwa muda wa muda wa miaka sita mpaka kumi na mbili kabla ya haijabilishwa tena.