Mwanzo / Huduma Zetu / BMH YAZINDUA KIKOSI KAZI KUPAMBANA NA UKATILI WA KIJINSIA NA UKATILI DHIDI YA WATOTO

BMH YAZINDUA KIKOSI KAZI KUPAMBANA NA UKATILI WA KIJINSIA NA UKATILI DHIDI YA WATOTO

BMH YAZINDUA KIKOSI KAZI KUPAMBANA NA UKATILI WA KIJINSIA NA UKATILI DHIDI YA WATOTO

Published on December 23, 2022

Article cover image

Disemba 22, 2022 Dodoma,

Hospitali ya rufaa Benjamin Mkapa ya jijini Dodoma imezidua kikosi kazi chenye jukumu la kutoa elimu juu ya unyanyasaji wa kijinsia na unyanyasaji wa Watoto.

Mkurugenzi Msaidizi wa Utafiti na Ubunifu Hospitalini hapo Bi. Hindu Ibrahim ambaye pia ni Mkufunzi wa kitaifa wa maswala ya unyanyasaji wa kijinsia alisema kuwa hatua ya kuzindua kikosi kazi hicho ni muhimu kwa wakaazi wa Mkoa wa Dodoma unaoshika nafasi ya pili nchini kwa kuwa na visa vingi vya ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya mtoto.

“Kikosi  kazi hiki kinaundwa na watumishi wa BMH kitasaidia kutoa elimu kwa wagonjwa wanaofika kupatiwa huduma, ndugu na jamaa wanoafika kusaidia ndugu wanaoumwa, pamoja wanaokuja kuona wagonjwa” alisema Bi. Hindu.

Katika uzinduzi huo wa kikosi kazi cha kupambana na ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya Watoto kulikuwa na washiriki kutoka makundi mbalimbali yanayoongoza mapambano ya kukomesha ukatili wa kijinsia ikiwemo, Ustawi wa jamii Mkoa, Dawati la Jinsia kutoka jeshi la Polisi, Klabu ya wanafunzi ya kupinga ukatili kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Bi. Josephine Mwaipopo, Afisa Ustawi wa jamii Mkoa wa Dodoma, ni miongoni mwa wageni waliyohudhuria na kufurahishwa na tukio hilo liloenda sambaba na uzinduzi wa vifaa vya hamasa na kitabu cha utaratibu wa kushughulikia visa vya ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya Watoto kwa watoa huduma Hospitalini hapo.

“Hospitali hii imekuwa daraja kwa waathirika wa ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto, na imekuwa msaada sana kwetu katika vita hii kwa kubaini waathirka na kutoa huduma za kiafya kwa waathilika. Alisema Bi. Josephine.

Tangu Juni 2022, Hospitali ya rufaa Benjamin Mkapa kwa ushirikiano na Wizara ya Afya, Shirika la Afya Duniani WHO, imekuwa ikitoa mafunzo mbalimbali kwa watumishi wake ya kuwajengea uwezo wa namna ya kuwabaini waathirika, kutambua namna bora ya kuwapatia huduma na kutoa elimu juu ya ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya Watoto. Tangu wakati huo zaidi ya visa 30 vya ukatili viliibuliwa miongoni mwa wananchi waliofika kupatiwa huduma.