Mwanzo / Huduma Zetu / DR MOLLEL AWASHUKURU TOKUSHUKAI MEDICAL GROUP

DR MOLLEL AWASHUKURU TOKUSHUKAI MEDICAL GROUP

DR MOLLEL AWASHUKURU TOKUSHUKAI MEDICAL GROUP

Published on March 17, 2023

Article cover image

Kauli hiyo imeelezwa na Naibu Waziri wa Afya, Dkt Godwin Mollel alipokutana na uongozi wa Shirika la afya la Japan, TOKUSHUKAI MEDICAL GROUP leo katika ofisi za wizara jijini Dodoma.

"Ninawashukuru kwa namna mlivyoungana na Hospitali ya Benjamin Mkapa na Chuo kikuu cha Dodoma, nchi ya Japani imekuwa ikisaidia katika sekta ya Afya hapa nchini" alisema Naibu Waziri.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Alphonce Chandika ameeleza jinsi TOKUSHUKAI MEDICAL GROUP ilivyo isaidia Hospitali ya Benjamin Mkapa.

"Hospitali ya Benjamin Mkapa imejengewa uwezo wa kufanya huduma ya upandikizaji figo na Shirika hili mpaka sasa tunajivunia kwa kupandikiza wenyewe hii ni kwasababu ya TOKUSHUKAI MEDICAL GROUP " alisema Dkt Chandika

Aidha mwenyekiti wa wa TOKUSHUKAI MEDICAL GROUP Prof. Higashiue Shinichi ameeleza jinsi walivyo pokelewa na taasisi hizi mbili UDOM na BMH

"Nasi tunashukuru kwa tulivyo pokelewa,kama tusingekubaliwa kutoa huduma hii leo tusinge kuwa hapa tukifurahia kuadhimisha miaka mitano ya upandikizaji figo" alisema Prof. Shinichi.