HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA NI YA KISASA NA INAYOJALI WAGONJWA
Published on June 25, 2024
Na Jeremiah Gasper Mbwambo, Dodoma, 23 Juni 2024.
Hayo yamesemwa na Mhe. Kassim Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipotembelea banda la Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) katika kilele cha wiki ya utumishi wa Umma jijini Dodoma.
"Nawapongeza kwa huduma mnazozitoa ni za kisasa na zinazingatia utu, hatujasikia unyanyasaji wala vitendo vya rushwa kwa kweli tunawapongeza sana endeleeni kufanya kazi" alisema Mhe. Majaliwa
Kwa upande wake Bi. Prisca Lwangili Mkurugenzi wa utawala na rasilimali watu akimkaribisha Waziri Mkuu ameeleza namna BMH ilivyo toa Huduma na Kutoa elimu kwa wananchi kupitia maonesho ya wiki ya utumishi wa Umma.
"Mhe. Kassim Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tunayofuraha kwa kututembelea katika banda letu pamoja na huduma zinazotolewa hapa na BMH tumeendelea kutoa elimu juu ya huduma ambazo Serikali imewekeza kwa kiwango kikubwa ikiwa ni pamoja na matibabu ya Sickle Cell, matibabu ya figo ambayo tunapandikiza figo, matibabu ya moyo, saratani, aidha tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa kwa Serikali chini ya Mheshimiwa Dr Samia Suluhu Hassan , Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha za kuanzisha jengo la matibabu ya saratani na huduma za upandizaji uloto ambazo ni za kitaifa na kimataifa " Alisema Bi. Lwangili
BMH imekuwa ikitumia maonesho kama sehemu ya kusogeza huduma zake kwenye Jamii ya watanzania.