Mwanzo / Huduma Zetu / MHE. UMMY MWALIMU (MB), WAZIRI WA AFYA AWASILISHA MAKADILIYO YA MAPATO NA MATUMI KWA MWAKA WA FEHDA 2023-2024

MHE. UMMY MWALIMU (MB), WAZIRI WA AFYA AWASILISHA MAKADILIYO YA MAPATO NA MATUMI KWA MWAKA WA FEHDA 2023-2024

MHE. UMMY MWALIMU (MB), WAZIRI WA AFYA AWASILISHA MAKADILIYO YA MAPATO NA MATUMI KWA MWAKA WA FEHDA 2023-2024

Published on May 12, 2023

Article cover image

Mhe. Ummy Mwalimu (Mb), Waziri wa Afya leo 11 Mei, 2023 amewasilisha makadilio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Afya kwa mwaka wa Fedha 2023-2024 katika vikao vya Bunge la Bajeti linaloendelea jijini Dodoma.

Mhe. Ummy Mwalimu ameliomba Bunge kuidhinisha kiasi cha Shilingi 1.2 trillion ili zitumike kutekeleza vipaumbele 14 vya sekta ya Afya kwa mwaka wa Fedha 2023-2024 akisema kuwa asilimia 59 ya fedha hizo zinatarajiwa kutumika katika shughuli za maendeleo na asilimia 41 yatakuwa matumizi ya kawaida kama shughuli za uendeshaji na kulipa mishahara ya watumishi wa sekta ya Afya.

Hotuba ya makadilio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Afya imesheheni pia taarifa mbalimbali kuhusu maboresho ya upatikanaji wa huduma za Afya nchini ikiwemo kuanzishwa kwa huduma za Kibingwa na Ubingwa Bobezi.

Ambapo, pamoja na mambo mengine amepigia chapuo Hospitali ya Rufaa ya Kanda Benjamin Mkapa ya Jijini Dodoma kwa kuanzisha huduma ya Upandikizaji wa Uloto kutibu watoto wenye ugonjwa wa Selimundu.

Akiomba dakika tano za kueleza kuhusu huduma hizo, Mhe. Waziri ametambua juhudi za Hospitali ya Benjamin Mkapa hasa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo Dkt. Alphonce Chandika katika kuanzisha huduma za kibingwa na ubingwa bozi akitolea mfano, hatua ya Hospitali hiyo kugharamia matibau ya watoto watatu waliyopandikizwa Uloto mapema Januari Mwaka huu.

Vile vile, aliitambua timu ya Madaktari bingwa na wataalamu waliyoshiriki kutoa huduma ya kupandikiza Uloto kwa namna ya pekee akiwataja Dkt. Stella Malangahe na Dkt. Jumanne Shakilu.