SERIKALI KUANZA NA RADIOLOJIA KATIKA TIBA MTANDAO
Published on March 24, 2023
Serikali itaanza na huduma ya radiolojia katika tiba mtandao (telemedicine) pale itakapoanza mwezi ujao.
Mkurugenzi wa TEHAMA kutoka Wizara ya Afya, Ndg Sylvanus Illomo, ameyabainisha hayo siku ya Alhamisi wakati wa majaribio ya programu katika Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) jijini Dodoma.
"Tiba mtandao itapunguza usumbufu kwa mwananchi kusafiri kufata huduma za matibabu mbali kwani ataweza kupata huduma za kibingwa katika mkoa alipo," alisema Mkurugenzi wa TEHAMA.
Ameyasema hayo leo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) jijini Dodoma wakati wa majaribio wa tiba mtandao.
Ndg Illomo aliongeza kuwa tiba mtandao itasaidia watalaamu wa afya kubadilishana uzoefu.
"Tiba mtandao itasaidia madaktari kujifunza kwa wenzao," alisema Ndg Illomo.
Amezitaja hospitali zitazoanza awamu ya kwanza ni BMH, MOI, Bombo ya Tanga na Hospitali ya Rufaa ya Morogoro