Mwanzo / Huduma Zetu / TUTALINDA MAZINGIRA , USAFI NA MIUNDOMBINU INAYOZUNGUKA BMH

TUTALINDA MAZINGIRA , USAFI NA MIUNDOMBINU INAYOZUNGUKA BMH

TUTALINDA MAZINGIRA , USAFI NA MIUNDOMBINU INAYOZUNGUKA BMH

Published on December 12, 2024

Article cover image

Na. Jeremiah Mbwambo, Dodoma 

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya BenjaminMkapa Prof. Abel Makubi 

"Wakati Tanzania inadhimisha miaka 63 ya Uhuru sisi tumeamua kuondoa magogo yaliyokuwa wamekwama kwenye daraja, daraja hili la BMH .Tunalifanyia usafi leo kwa sababu ni daraja muhimu kwetu watumishi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa na wananchi wote wanaokuja kupata huduma hivyo ni lazima kuhakikisha maji yanapita vizuri chini bila kuziba na  kusababisha maji kupita juu hivyo kufunga njia” Alisema Prof.  Makubi 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Hospitali ya Benjamin Mkapa Bi. Prisca Lwangili amesema 

"Uzalendo ni pamoja na kujali Rasilimali za nchi hivyo nasi watumishi wa Hospitali tumeona wakati tunapo adhimisha miaka 63 ya Uhuru tumeamua kuungana kwa pamoja kufanya usafi kwenye maeneo yanayo pita maji mengi hususani kwenye madaraja yaliyo karibu na  Hospitali ya Benjamin Mkapa " alisema Bi.  Prisca

Aidha, Daktari Bingwa wa mfumo wa mkojo Remidius Rugakingila amesema afya ya kweli inaanza na kutunza mazingira. 

"Mazingira yasipokuwa salama inaweza kutupelekea kuwa na afya mbaya na kupata ajali kama daraja hili lisipo safishwa uchafu unaweza kujaa na maji yakavunja daraja hivyo nimefurahi kuona nasi tunasimama na jamii kuboresha mazingira" alisema Dkt. Remmy

Wakati taifa linaazimisha miaka 63 ya Uhuru,  watumishi wa hospitali ya Benjamin Mkapa wameadhimisha kwa kusafisha mazingira yanayo wazunguka, ikiwa ni pamoja na kuondoa uchafu uliyokuwa umekwama kwenye daraja la BMH.