Mwanzo / Kurasa / Afya ya Meno na Kinywa

Afya ya Meno na Kinywa

Afya ya Meno na Kinywa

Published on September 27, 2022

Idara Afya ya kinywa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa hutoa huduma za matibabu ya kinywa  kwa watoto na watu wazima  kama ifuatavyo;

  • Uzibaji wa jino wa kawaida (jino lenye tundu dogo au lenye mashambulizi kidogo)
  • Uzibaji wa jino wa kuua kiini cha jino (Jino lenye tundu kubwa au la muda mrefu)
  • Kung'oa jino lisilofaa kuziba (Jino lililoota sehemu isiyo sahihi au lilliloota vibaya, Jino lililokana kuota likasalia katika mfupa na kuleta athari)
  • Kuweka meno bandia (ya kuvaa na kuvua au ya kuvaa moja kwa moja)
  • Upasuaji Taya na Vivimbe kwenye taya (inahusisha upasuaji mdogo au mkubwa)
  • Usafishaji meno yenye uchafu
  • Upangaji meno

Huduma zote hizi hutolewa na Madakari Bingwa wa Kinywa na Meno na wataalamu wenye uzoefu kwa kutumi vifaa tiba vya kisasa na kuhakikisha huduma za KInywa na Meno

Katika Hospitali ya Benjamin Mkapa zinatolewa kwa kiwango cha ubora ngazi ya kimataifa.