Mwanzo / Huduma Zetu / WATUMISHI WA HOSPITAL YA BENJAMIN MKAPA KUFANYA MAZOEZI PAMOJA KILA WIKI

WATUMISHI WA HOSPITAL YA BENJAMIN MKAPA KUFANYA MAZOEZI PAMOJA KILA WIKI

WATUMISHI WA HOSPITAL YA BENJAMIN MKAPA KUFANYA MAZOEZI PAMOJA KILA WIKI

Published on July 05, 2024

Article cover image

Na Ludovick Eugene Kazoka, Dodoma

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), Prof Abel Makubi, leo amezindua rasmi programu ya mazoezi ya pamoja kwa watumishi wote wa BMH.

Akiongea na watumishi wakati wanapasha viungo, Prof Makubi, amesema kuanzisha mazoezi ni utekelezaji wa agizo la Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa Wananchi kufanya mazoezi.

"Mazoezi ni afya na yanasaidia kuzuia magonjwa ambayo siyo yakuambukiza. Hii ni kuonyesha mfano kwa taasisi nyingine za umma, tunaonesha kwa vitendo maelekezo ya Makamu wa Rais na Miata Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kitutaka kufanya mazoezi ili kuepukana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza" amesema Prof Makubi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa BMH, Prisca Lwangili, amesema programu hii itakuwa inafanyika mara moja kwa wiki.

"Tuna timu ya michezo hapa inayojulikana sana inaitwa BMH Sports na inashiriki mashindano mengi ya michezo," amesema Bi. Lwangili, wakati akimkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa BMH kuongea na watumishi walioshiriki mazoezi hayo.

Mmoja wa watumishi walioshiriki mazoezi hayo, Ndg John Mwaluko, amesema amepata hamasa sana kuona Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali akiongoza programu hii ya mazoezi.

"Nitakuwa nikishiriki kila wiki haya mazoezi ili kuzuia magonjwa yasiyo ya kuambukiza," amesema Ndg   Mwaluko kutoka Kitengo cha Upandikizaji Uloto, BMH.

Mtumishi mwingine aliyeshiriki mazoezi hayo, Devotha Lutandula, amesema, 

"Sisi kama wanamichezo wa BMH tunamshukuru Mkurugenzi Mtendaji, Prof Makubi kwa kuanzisha programu hii kwani itatusaidia kuwa imara muda wote." alisema Devotha