Radiolojia ya Uchunguzi na Upigaji Picha

Idara ya Radiolojia ya Hospitali ya Benjamin Mkapa ni nguzo muhimu ya huduma za uchunguzi na tiba kwa njia ya picha, ikiwa na mchango mkubwa katika huduma kwa wagonjwa kutoka fani zote za kitabibu. Tangu kuanzishwa kwake, idara hii imekua na kuwa kituo cha kisasa kinachotoa huduma mbalimbali za upimaji na tiba kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu. Ikiwa na wataalamu waliobobea wakiwemo madaktari wa radiolojia, mafundi sanifu na wataalamu wa tiba kwa picha, idara hii huchangia katika utambuzi sahihi, mipango ya matibabu, na ufuatiliaji wa tiba kwa wagonjwa wa nje na wa ndani.
Huduma za Idara
1. Radiolojia ya Uchunguzi:
Tunatoa huduma mbalimbali za upimaji kwa kutumia vifaa vya kisasa vya uchunguzi ili kusaidia madaktari kufanya maamuzi sahihi ya kitabibu. Huduma hizi ni pamoja na:
• X-Ray na Fluoroscopy: Picha za kawaida, vipimo vya kutumia dawa za mcontrast (mfano barium, hysterosalpingography), na taratibu zinazoongozwa na fluoroscopy.
• Ultrasound: Ikiwemo uchunguzi wa tumbo, mimba, magonjwa ya akina mama, mishipa ya damu, na misuli na mifupa.
• Mammography: Upimaji wa kidigitali wa matiti kwa ajili ya kugundua mapema saratani au matatizo mengine ya matiti, ukiambatana na biopsy inapohitajika.
• CT Scan (Computed Tomography): Upigaji picha kwa viwango vingi kwa ajili ya uchunguzi wa majeraha, saratani, magonjwa ya moyo na mishipa, na mfumo wa fahamu, pamoja na CT angiography na upasuaji unaoongozwa na CT.
• MRI (Magnetic Resonance Imaging): Upigaji picha wa ubora wa hali ya juu kwa uchunguzi wa ubongo, mfumo wa fahamu, misuli na mifupa, nyonga, na tumbo kwa kutumia MRI ya 3 Tesla.
• CT IVU na Triphasic Liver Studies: Vipimo vinavyofanyika mara kwa mara kusaidia huduma za magon