Bunge Logo
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Bunge la Tanzania

Habari

Mkutano wa Kumi na Nane wa Bunge waanza Jijini Dodoma


Mkutano wa Kumi na Nane wa Bunge umeanza Jijini Dodoma siku ya Jumanne tarehe 28 Januari, 2025 na unatarajiwa kumalizika tarehe 14 Februari, 2025 Jijini Dodoma. Mkutano huu ni mahsusi kwa ajili ya Kamati za Kudumu za Bunge kuwasilisha Taarifa za Mwaka za Shughuli za Kamati kwa kipindi cha Januari 2024 hadi Januari 2025. Aidha katika Mkutano huu, Bunge linatarajia kujadili na kupitisha Miswada mitano (5) ya Sheria ambayo ilisomwa Mara ya Kwanza katika Mikutano iliyopita.

Miswada hiyo ni:-

i. Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na.3) wa Mwaka 2024 [The written Laws (Miscellaneous Amendments) (No.3) Bill 2024];

ii. Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na.4) wa Mwaka 2024 [The written Laws (Miscellaneous Amendments) (No.4) Bill 2024];

iii. Muswada wa Sheria ya Shirika la Utangazaji Tanzania wa Mwaka 2024;

iv. Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Usimamizi wa Mazingira wa Mwaka 2024 [The Environmental Management (Amendments) Bill, 2024]; na

v. Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Kazi wa Mwaka 2024. [The Labor Laws (Amendments) Bill, 2024].

Kwa upande mwingine wastani wa Maswali ya Kawaida 250 yanatarajiwa kuulizwa na Wabunge na kupatiwa majibu na Serikali. Aidha, kutakuwa na maswali ya papo kwa papo kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa siku za Alhamisi.