Mamlaka
Bunge la Tanzania ni Mhimili ambao Mamlaka na Majukumu yake yametajwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1997, Sura ya Tatu.
Ibara ya 63(1) ya Katiba inaeleza kwamba Bunge ndicho Chombo Kikuu cha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambacho kitakuwa na madaraka kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekekezaji wa majukumu yake yaliyotajwa katika Katiba