Muundo
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linajumuisha aina za wabunge zifuatazo (Ibara ya 66 ya Katiba):
- Wabunge waliochaguliwa kuwakilisha majimbo ya uchaguzi;
- Wabunge wanawake wa idadi inayoongezeka, kuanzia asilimia ishirini ya Wabunge waliotajwa katika aya ya (1), (3) na (4), watakaochaguliwa na vyama vya siasa vinavyowakilishwa Bungeni, kwa mujibu wa ibara ya 78, na kwa kuzingatia masharti ya uwiano wa uwakilishi baina ya vyama hivyo;
- Wabunge watano waliochaguliwa na Baraza la Wawakilishi kutoka miongoni mwa wajumbe wake;
- Mwanasheria Mkuu;
- Wabunge wasiozidi kumi walioteuliwa na Rais.
Uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 ulitoa aina na idadi ya wabunge:
Aina ya Wabunge | Idadi | |
1 | Wabunge waliochaguliwa kuwakilisha majimbo ya uchaguzi.(Tanzania Bara 214 na Zanzibar 50) | 264 |
2 | Wabunge wa viti maalum | 113 |
3 | Wabunge waliochaguliwa na Baraza la Wawakilishi | 5 |
4 | Mwanasheria Mkuu. | 1 |
5 | Wabunge walioteuliwa na Rais | 10 |
Jumla | 393 |