Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Mifugo na Uvuvi

Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA)

Kampasi ya Mbegani

Kuhusu FETA Mbegani

FETA Mbegani, ambayo awali ilijulikana kama Kituo cha Maendeleo ya Uvuvi cha Mbegani (MFDC), ilianzishwa na Serikali mwaka 1966 kama kituo cha maendeleo ya uvuvi wa jadi. Lengo kuu lilikuwa kuhamasisha na kuchochea uboreshaji wa teknolojia ya vyombo vya uvuvi ili kuongeza uimara wake baharini, pamoja na kubuni na kutengeneza zana bora za uvuvi kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa upatikanaji wa samaki.

Mwanzoni mwa mwaka 1970, MFDC ilibadilishwa kuwa taasisi rasmi ya mafunzo ya ufundi ili kuwahudumia wanafunzi wa cheti cha uvuvi waliokuwa wakisoma katika Taasisi ya Mafunzo ya Kilimo ya Wizara ya Kilimo (MATI) – Nyegezi.Uhamisho huo ulifanyika kufuatia mabadiliko ya kimuundo ya wizara, ambapo Idara ya Uvuvi ilihamishiwa kutoka Wizara ya Kilimo na Ushirika kwenda Wizara ya Maliasili.Kituo hicho kilipanuliwa zaidi mwishoni mwa miaka ya 1970 ili kuanzisha programu za stashahada katika ujenzi wa boti, uchakataji wa mazao ya uvuvi, uhandisi wa baharini na teknolojia ya uvuvi. Katika kipindi hicho, wanafunzi waliokuwa wakisomea programu ya cheti Mbegani walihamishiwa Nyegezi ili kutoa nafasi kwa mchakato wa upanuzi. Wanafunzi hao kwa hakika walikuwa waanzilishi wa programu za mafunzo katika Taasisi ya Taifa ya Mafunzo ya Uvuvi (NFFI).

Mnamo mwaka 2010, MFDC ilibadilishwa kuwa Kampasi ya FETA Mbegani na kuwa Makao Makuu ya FETA. FETA Mbegani imesajiliwa na kupata ithibati ya NACTVET kwa namba ya usajili REG/ANE/002 ili kutoa mafunzo mbalimbali katika teknolojia za uvuvi na ufugaji wa viumbe kwenye maji katika ngazi ya Astashahada na Diploma (ngazi ya IV, V, na VI).  

Kozi zinazopatikana katika Kampasi yetu ya Mbegani

Kozi Ndefu.

  1. Ufugaji Viumbe kwenye Maji
  2. Uchakataji wa Samaki, Udhibiti wa Ubora na Masoko
  3. Usimamizi wa Mazingira na Rasilimali za Majini
  4. Uvuvi na Ubaharia
  5. Uhandisi wa Mitambo Bahari na Upoozaji

Kozi Fupi.

  1. Usimamizi wa Ubora, Usafi wa Viwandani na Usafi wa Mazingira
  2. Ukusanyaji na Uhifadhi wa Samaki
  3. Ujenzi wa Vyombo vya Kuhifadhia Vyenye Insulation
  4. Uchakataji wa Samaki wa Kiwandani
  5. Ufundi wa Injini Ndogo za Majini
  6. Teknolojia ya Nyavu na Usimamizi wa Vyombo vya Uvuvi
  7. Uendeshaji wa Staha na Utaalamu wa Baharini
  8. Uendeshaji, Matengenezo na Ukarabati wa Injini Ndogo za Nje
  9. Kozi Maalum kwa Wanawake katika Uvuvi
  10. Kozi Maalum kwa Wavuvi Wadogo
  11. Usimamizi Shirikishi wa Uvuvi
  12. Ufugaji Samaki
  13. Kuogelea na Uokoaji
  14. Mafunzo ya BMU juu ya Usimamizi wa Rasilimali Asilia
  15. Kozi Maalum Zinazotolewa kulingana na Mahitaji ya Mteja

Mahali Kampasi Inapopatikana

Kampasi ya Mbegani ipo kilomita 6 kutoka barabara kuu ya Bagamoyo mtaa wa Zinga kwa Mtoro, kandokando ya Bahari ya Hindi, katika wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani

  • Mratibu wa Mafunzo:       Greyson Kissai,0713428822, greyson.kissai@feta.ac.tz
  • Mawasiliano ya Ofisi ya Udahili: 0713088755, admission.mbegani@feta.ac.tz
  • Mawasiliano ya Ofisi ya Mitihani: 0714145514 / 0763145515 , hassani.mhando@feta.ac.tz
  • Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma:  Merisia Mparazo, 0787217651, merisia.mparazo@feta.ac.tz
  • S.L.P 83,  Bagamoyo, Pwani.
  • Barua Pepe:mbegani@feta.ac.tz